Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala)
(( شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ))
((Mwezi wa Ramadhaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uongofu na upambanuzi)) [Al-Baqarah: 184]
Kwa hivyo basi ndugu Muislamu, jitahidi ufanye ibada hii usome na kuhifadhi Qur-aan kwa wingi kabisa kwani thawabu na fadhila zake ni nyingi na adhimu mno kama tunavyozinukuu humu. Pia jitahidi uweze kuhitimisha (kumaliza kuisoma) japo mara moja Qur-aan nzima kabla ya mwezi wa Ramadhaan kwisha.
No comments:
Post a Comment